Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) - Susan Davis (free ebook reader for iphone .TXT) 📗
- Author: Susan Davis
Book online «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) - Susan Davis (free ebook reader for iphone .TXT) 📗». Author Susan Davis
Mathayo Mtakatifu 24:37-39. Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya gharika watu walivyokuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
Kwa hivyo wana, amkeni! Itwaeni zawadi hii yenye thamani, ambayo nawapa na mniruhusu nigharamie uhuru wenu. Ninaweza. Ninataka. Ni yangu kuwapa na ninawapa bure. Ni raha yangu kuwafanya muwe wazima, wenye amani na fahamu nzuri. Haya yote ni yenu ikiwa mtanijia na kujitolea kikamilifu. Mnipe uzima wenu. Niacheni niwe Bwana wenu. Niacheni niwajaze na Roho wangu na niwanifunike na damu yangu ndipo nifute orodha ya dhambi zenu.
Luka Mtakatifu 17:16. Akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
Niacheni niwaonyeshe njia mtakayoitembelea ili muachilie njia za adui. Njooni kwangu na mpokee mioyo iliyotakaswa na kuoshwa kwa moto na maji ya neno langu. Ni yenu kutwaa.
Yohana Mtakatifu 15:3. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.
Achaneni na mipango yenu yote na mnipe maisha yenu, na mipango yenu yote. Nipeni maisha yenu. Nitayabadili maisha yenu na mipango yenu na mipango ambayo nilipanga tangu hapo awali kuhusu maisha yenu, nilipowaumba. Tembeeni katika mapenzi yangu. Msitende dhambi kwa kutembea kwenye njia na hiari zenu. Njooni kwenye mapenzi yangu ili muwe wakamilifu mbele zangu. Hii ndiyo hamu yangu kuhusu maisha yenu.
Mimi ni muumba wenu. Najua yaliyo bora kwenu. Njooni mpokee zawadi hii kuu—amani kwa muumba wenu. Wana, saa inayoyoma. Msipoteze wakati kufanya uamuzi wa kunifuata. Wakati huu ni muhimu. Sitaki mkumbane na wakati mgumu ujao duniani. Nifuateni na nitawaonyesha ukweli na kuyafungua macho yenu. Nitayafungua macho yenu kwa kuyatoa magamba machoni na kuwapa uhuru, na kuwaandaa ili mje nyumbani ili muwe salama nami.
Matendo ya mitume 9:17-18. Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani, akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa.
Nataka kuwaamsha. Hii ni hamu yangu. Mje mikononi mwangu. Msisite. Kusitasita ni hatari na kunaweza kuwafanya mpoteze wokovu wenu.
Maneno haya yanatoka kwa BABA ambaye anawajali na kuawapenda, YAHUSHUA.
SURA YA 27: HAMNA BUDI KUJITAYARISHA IKIWA MNATAKA KUJA NAMI
Natuanze. Wana, huyu ni BWANA wenu na nina maneno ya kuwanenea. Wakati unaisha. Hivi karibuni nitamjia bi arusi wangu ili nimlete mahali palipo salama. Atainuka kutoka duniani kwa ushindi na utukufu. Yeye ni mshindi wangu. Nitamleta kwangu na kumuinua ili tukutane hewani. Tukio hili linaitwa ‘Unyakuo’ au cho chote kile utakachoamua kuliita tukio hili. Hili tukio litatendeka hivi karibuni. Nitamvuta bi arusi wangu kutoka kwa minyororo ya dunia ambayo inaenda kombo – bila muelekeo; dunia ambayo inaishi mbali na MUNGU.
1 Wakorintho 15:51-52. Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
Mimi ni MUNGU anayezuia matukioa mabaya duniani, na sasa dunia itaanza kuona maisha yatakavyokuwa bila mkono wangu mkuu wa ulinzi. Hivi karibuni yatatendeka. Wengi watashuhudia tukio hili kama wale walioachwa. Wachache watalishuhudia kama wale watakaochukuliwa kutoka duniani. Nataka muwe kati ya wale watakaochukuliwa kutoka duniani, ila ni sharti mjitayarishe ikiwa mnataka kutoka nami. Ni wale tu ambao wamejiosha na kuwa weupe kwa damu yangu ndio watakao kuja nami, nitakapo mwita bi arusi wangu juu. Ni wachache sana wanaokuja. Hii ni hatari, wanangu. Wengine wote watawachwa nyuma.
1 Yohana 1:7. Basi tukienda nuruni kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
Ni huzuni ulioje uwangojeao watakaoachwa nyuma! Usiwe mmoja wao. Si lazima uwe mmoja wao. Niwatengenezea njia. Nimewatengenezea mahali pa kupitia. Ni kupitia kwa damu yangu.
Njia yako ni wazi na huru kupitia kwangu. Hakuna njia nyingine. Hakuna mwingine atakayewaokoa. Hakuna majibu kwingine. Ni hili tu: Njooni kwangu, na mjitolee kwangu. Msisite. Fanyeni hima kwa maana kurudi kwangu ku karibu. Kuweni na wakati wa kunijua mimi. Ni tayari na ninawasubiri. Upendo wangu wawangojea. Njooni kwangu kwa toba na unyenyekevu. Nitawatayarisha kupitia kuwafunika kwa damu yangu, na neno langu—kuoshwa kwa neno langu.
Waefeso 5:25-27. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyazi wala lo lote ka hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Njooni kwangu. Msipoteze wakati. Hii ndiyo saa ya kumchukua Mungu bila utani. Msingojee sana. Ni mimi BWANA MUNGU YAHUSHUA
SURA YA 28: UZIMA WENU WA MILELE U MASHAKANI
Natuanze tena. Wakati wa u karibu wa kurudi kwangu. Unatimia. Kuna mengi mnayohitaji kufanya ili mjiandae. Nina mengi ninayotaka mfanye. Nawataka mjitolee kwangu na myatoe maisha yenu kwangu kikamilifu. Nataka mniachie kila kitu. Kujitolea nusu ni kama kukosa kujitolea. Myatafakari haya sana. Uzima wenu wa milele u mashakani. Bila kujitolea kikamilifu, ninyi si wangu. Haijalishi mnayoyasema au kufikiria. Ni kwa kujitolea kikamilifu ndiko kutakako dhihirisha kuwa mu wangu. Mkiangalia kushoto na kulia, mtapotoshwa. Msiwe hivyo. Muda unayoyoma. Wanangu, ni sharti muamke! Muwe macho!
Mathayo Mtakatifu 7:14. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Wakati waja wa kumuondoa bi arusi wangu, kumleta nyumbani, kumsindikiza nyumbani kwake kupya ambako ataishi nami milele, BWANA ARUSI WAKE. Natamani kumkumbatia, kumshika kwa karibu, kumpa mapenzi yangu, kumuhusudu na kumuonyesha mapenzi yangu. Hivi karibuni haya yatatendeka. Ni tayari na bi arusi wangu pia yu tayari. Ananisubiri kwa ustahamilivu. Bi arusi wangu ndiye nuru ya dunia. Anang’aa katika dunia yenye giza, na isiyopendeza. Yeye ndiye nuru ya mwisho. Nuru yake ni kuu na inaonyesha nuru yangu. Nuru ni ukweli—ukweli wangu unaodumu milele. Mengine yote ni uongo kutoka kwa adui wangu. Ameukanganya ulimwengu na uongo wake. Ulimwengu umedanganyika na watu hawauoni ukweli.
Yeremia 17:5-6. BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu Yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, na moyoni mwake amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
Wakati umewadia wa wanangu kuamka na kuukabili ukweli. Dunia inaisha. Kipindi kipya chaja: kipindi cha Mpinga Kristo na mabadiliko magumu yatafuata. Hakuna yeyote atakayekua salama, ila tu wafuasi wangu wa kweli ambao nitawapeleka nyumbani na kuwaweka mahali pa usalama. Hawa pekee ndio walio na ruhusa ya kutoshiriki kwa matukio yajayo—yale ambayo dunia itakumbana nayo pindi tu adui wangu ashikapo usukani na kuruhusiwa kutawala na kutamalaki. Ni siku ya huzuni tele.
Ufunuo 17:16-17. Na zile pembe kumi ulizoziona na huyo mnayama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto. Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe.
Huu utakuwa wakati mgumu sana kwa wanadamu. Shida kubwa yaja duniani. Saa hii yaja na yaja kwa kasi. Hivi karibuni, mambo yatabadilika. Nawataka ninyi wana mjitayarishe ili mwende juu nami. Nawataka mje nami. Mwaweza kuyaepuka haya yote ikiwa mtayafungua macho na kuja kwangu kwa unyenyekevu, toba na kujitolea. Natamani kuwachukua mikononi mwangu na kuwaokoa kutokana na simanzi ijayo. Hamu yangu kuu ni kuwaokoa kutoka kwa matatizo yajayo. Nawapa maneno mengi na ishara nyingi za kuwaleta kwa ukweli huu. Ni wachache sana wanaonisikiza. Wengi wangali wameolewa na dunia hii ya uovu ambayo ni kahaba. Ndiyo, wana. Ikiwa mngali mumeshikilia dunia na njia zake, mnafanya usherati kwangu na sitawaleta katika ufalme wangu. Kwa hivyo, ondokeni kwa dunia na njia za dunia. Dunia ni chafu bila maadili na yampinga Mungu, na siwezi kustahamili tena.
Ezekieli 16:35. Kwa sababu hiyo, Ewe kahaba, lisikie neno la BWANA; Bwana MUNGU asema hivi: Kwa sababu uchafu wako umemwagwa, na uchi wako umefunuliwa, kwa njia ya uzinzi wako pamoja na wapenzi wako; na kwa sababu ya vinyago vyote vya machukizo yako; na kwa sababu ya damu ya watoto wako, uliyowapa.
Wakati unaisha. Rudini kwa fikira zenu. Yafungueni macho yenu. Ziangalieni nyakati muishimo. Msidanganywe na yale myaonayo na kudhani kuwa kila kitu ki sawa. Nitawaleta ufalmeni mwangu na kwa uzima wangu wa milele. Jitoleeni kwangu. Nifanyeni niwe BWANA na MUNGU wenu. Wakati wa kuamua ni sasa. Msichelewe! Huyu ni BWANA wenu, YAHUSHUA.
Luka Mtakatifu 21:31-32. Nanyi kadhalika mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu. Amin, nawaambieni, kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie.
SURA YA 29: NI SHARTI MNIKIMBILIE SASA WALA SIO KUTEMBEA
Ndiyo binti, natuanze. Wanangu, huyu ni BWANA wenu anayezungumza nanyi. Nataka mjue ya kuwa naja hivi karibuni. Saa i mlangoni. Hivi karibuni, nitakuja kumchukua bi arusi wangu. Apendeza, uzuri wake wang’aa. Namwangalia kwa hamu na ninataka kumleta nyumbani kwa makao yake yaliyorembeka ambayo nimemwandalia. Saa hii inakimbia wanangu. Yafaa mjitayarishe. Yafaa mjiandae kwa upesi. Siku ya huzuni yaja. Hivi karibuni nitambeba bi arusi wangu. Nitampeleka kwa usalama. Ni dakika chache tu zilizosalia. Kurudi kwangu kwakaribia mlangoni. Kwa hivyo njooni mikononi mwangu. Ni karibu sana. Ni sharti mnikimbilie wala sio kutembea mkinijia. Msiwe walegevu wana. Myatilie maonyo yangu maanani. Nawalete mahali hapa. Wanangu, nawataka muamke, muutazame ukweli. Hivi karibuni saa hii itakuwa mlangoni. Nisikizeni wana, nawataka muamke. Kuna matatizo ambayo yaja, duniani. Yaja kama gari la moshi. Yateremka kwa kasi. Hakuna liwezalo kuyakomesha. Hakuna mwanamume, mwanamke, mtoto awezaye kukomesha yajayo. Kutakuwa na matokeo makali, kwa watakaokataa kuyasikiza maonyo yangu. Nimewaonya kwa njia ya ishara nyingi. Hakuna atakayekuwa na hudhuru ya kusema kwamba hakujua. Kila mmoja atawajibikia dhambi zake—jinsi nilivyosema katika kitabu changu.
Warumi 14: 12. Basi ni hiyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.
Mnaamua kucheza na dunia ila mjue kuwa sio kila kinga’acho ni dhahabu, wanangu. Dunia inang’aa na kuonekana mpya ila ni sumu tupu na yawapa kifo. Iwekeni dunia kando na kumtazama MUNGU wenu. Je, sistahili kufuatwa miye?
Yohana 12:25. Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalamisha hata uzima
Comments (0)