Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) - Susan Davis (free ebook reader for iphone .TXT) 📗
- Author: Susan Davis
Book online «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) - Susan Davis (free ebook reader for iphone .TXT) 📗». Author Susan Davis
Dunia imeanza kuona athari za kumkana Mungu wake. Kuna matokeo unapoamua kumkana Mungu. Kuna matokeo magumu. Sifurahishwi na wale ambao wanasonga karibu nami kisha tena wanaukimbilia ulimwengu kwa sababu wanaamini kuwa ulimwengu ni chaguo nzuri kuniliko mimi. Hili si jambo la busara hata kidogo. Ilhali hivi ndivyo walimwengu wanafanya: kuacha matumaini na kukimbilia dunia ambayo inawafanya wajitegemee, wajisimamie, wawe na ubinafsi, na kutafuta njia zao wenyewe. Wakati wangu wa kurudi umewadia. Je wanangu, mu wapi? Mu nami an na ulimwengu? Dunia haina matumaini yote. Ni dunia ambayo inaaguka, dunia iliyopotea. Imepotea kwa maana haitafuti Mungu ili awape majibu kuhusu maisha.
Mapepo sasa yanatawala ulimwengu kupitia njia nyingi: kupitia ujumbe mnaoupata, kupitia mfumo wa dunia ambao umewekwa sasa hivi na kupitia makanisa ambayo yamepotea. Neno langu tu ndilo la kweli na la kutegemewa. Halibadiliki. Kuweni na wakati nami. Muombeni Roho wangu awafunulie ukweli. Atawafunulia ikiwa mtamuuliza katika haki. Anatamani kuwaonyesha ukweli. Hii ndio tamaa yake kuu. Awaonyeshe ukweli ili mweze kuoshwa na neno langu.
1 Wakorintho 2:13. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.
Wanangu, msiruhusu dunia iwazibe macho yenu. Msiruhusu adui awapoteze kama alivyowapoteza wengi. Muwe macho. Njooni kwenye nuru yangu. Mlishwe kwa ukweli wangu na kwa mkono wangu mtakatifu. Natamani kuwalisha ukweli, kuwastawisha na mafunzo yangu kutoka kwa neno langu. Acheni niwalete katika nuru yangu. Niwaonyeshe yale ambayo hamjayaelewe hapo awali. Nina mengi ya kuwambia. Nataka kuwavuta kutoka gizani. Huu ndio wakati wa ukweli kujulikana. Siyo ukweli ulio hafifu, uliokamilika. Msichezee wokovu wenu.
Kwa hivyo njooni kwangu. Ulilieni ukweli. Nitawapa ukweli; ukweli usiobadilika.
Sasa wana, sasa ndio wakati.
Mimi ni YAHUSHUA, MUUMBA VYOTE.
SURA YA 16: SAA YA KURUDI KWANGU INAKARIBIA
Tuanze, binti. Saa ya kurudi kwangu wanangu yaja. Saa hii inakaribia kama vile mchana hugeuka kuwa usiku. Naja na hakuna lolote litakalo weza kusimamisha tukio hili.
Yafaa mzingatie sana umuhimu waa tukio hili. Tukio hili litaathiri kila mtu. Hakuna ye yote ambaye hataathiriwa ulimwenguni kote. Kutakuwa na wale watakaoepuka na kwenda nami kwa raha na kuna wale ambao watabaki na kuangamia.
Jinsi utakavyo patikana wakati wa tukio hili ni chaguo lako. Jinsi utakavyoathiriwa na tukio hili ni chaguo lako. Utaenda nami nirudipo kuchukua bi arusi wangu kumpeleka mahali pa salama ama utabaki na kuangamia nimwagapo gadhabu yangu kwa adui wangu?
Chaguo hili linaonekana rahisi ila kuna wachache tu ambao wanachagua kwenda nami. Ni wachache sana wanaonitazamia au wanao amini kuwa kurudi kwangu ku karibu. Mbona hivi wanangu? Ni kwa sababu dhambi imewabana. Wameuzoea na kuukubali ulimwengu huu uliojaa dhambi. Wanazipenda njia za dunia na wazikumbatia haraka na kwa upesi. Hawasomi neno langu, wala kuliamini. Hawanitazami ili niwape majibu wanayohitaji. Dunia na binadamu ndio washauri wao.
Wana, siwezi kuwaokoa wale wasionirudia kwa unyenyekevu, kwa imani kama ya moto. Bila kujitolea kwangu kikamilifu, sitaweza kuwaokoa nitakaporudi ili kumchukua bi arusi wangu. Bi arusi atachukuliwa nanyi mtaachwa. Wale wanangu watakaoachwa watakabiliana na adui. Utakuwa wakati mgumu sana. Hakutakuwa na usaidizi kutoka kwangu.
Marko Mtakatifu 10:15. Amini, nawaambieni, yeyote asiyekubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa.
Mngali mna nafasi ya kurudi kwangu katika siku hizi za mwisho kabla ya kurudi kwangu. Mkijitolea kwangu, mnipe hiari zenu nitawafanya watu wapya na kuwatayarisha kuingia kwa ufalme wangu.
Ninaona ni wachache sana wanotaka kufanya hivyo. Ni idadi ndogo sana ya watu wanaonifuata jinsi ninavyotaka. Ni wachache sana wanaonipa maisha yao. Wengi wanaamini dunia na fikira za binadamu.
Wanangu, nawataka mjirudi na kuacha upumbavu. Mimi tu ndiye niwezaye kuwasaidia. Hakuna mahali pengine popote pa kwenda. Ndiyo, mnaweza kurudia dunia lakini dunia inaisha na inazorota kila siku.
Nawataka muwe uzimani. Msidanganywe na yale mnayodhani ni ya kawaida. Myaonayo kwa macho yaweza kuwahadaa. Dunia haiwezi kuendelea bila mimi. Mimi ndiye dira ya uadilifu. Bila mimi, dunia itakosa uadilifu.
Wanangu, hivi karibuni, na ni karibu sana, nitarudi. Sitaki muachwe au mpotee. Nawataka mje nami. Huu ndio mualiko wangu kwenu. Nawataka mje nami. Mtembee kwenye njia nyembamba nami. Niacheni niwaongoze. Ushikeni mkono wangu.
Msikose nafasi hii kubwa ya kuwa bi arusi. Ni mrembo na amejitayarisha. Nampenda mno. Ni kanisa langu linipendalo kuliko vyote. Ananishuhudia. Mimi ni wake wote. Naja kumuokoa kutokana na tisho lijalo. Hataathiriwa na yote yatakayotokea. Nitamtwaa mikononi mwangu.
SURA YA 17: KUHUSU MPINGA KRISTO
Tuanze. Wanangu, ningependa kuzungumzia kitu kipya leo: Nataka kuzungumzia juu ya mpinga Kristo na utawala na mamlaka yake ulimwenguni.
Hivi karibuni, atakuja ulimwenguni ili kuutawala na kutamalaki. Kila kitu kitageuka. Utakuwa wakati usio na matumaini kwa wengi.
1 Yohaha 2:22. Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana.
Wale watakao litaja jina langu watapatikana na makosa. Jina langu litamaamisha kifo. Wengi wanaodai kunijua wataogopa kulitaja jina langu. Hii itatendeka duniani kote. Maangamizo yatakuwa kote duniani. Yatakuwa maangamizi ya kina.
Ufunuo 20:4. Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu, nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.
Mpinga Kristo atakuja wakati ambapo dunia itakuwa inatafuta majibu na suluhisho kwa ajili ya uharibifu utakaokuwa baada ya bi arusi kunyakuliwa. Hili tukio litatendeka hivi karibuni. Dunia itaona shida isiyolinganishwa na nyingine yote.
1 Yohana 4:3. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
Mpinga Kristo atajaribu kuwaangamiza wote wanaoshika njia zangu na ushuhuda wangu. Mpinga Kristo ataleta ile chapa ya mnyama kama njia yake ya kwanza ya kuwadhibiti watu.
Wale watakao kataa kuwekwa chapa ya mnyama wataangamizwa kama wapinzani wa mfumo wake. Wale watakaopewa chapa watawakejeli wale ambao wataikataa. Wale watakaokubali chapa watapotea milele. Hiyo ni miliki ya mfumo wa mpinga Kristo.
Ufunuo 14:11. Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wasujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.
Wanangu, yafaa mzingatie sana maonyo haya bila kuyapuuza. Haya yatatimia hivi karibuni.
Wakati wangu wakumchukua bi arusi yangu umefika. Kanisa langu lililo kweli. Wakati huu umewadia kwa maana mfumo wa mpinga Kristo u karibu kuanza.
Mpinga Kristo anakuwa mkatili na mwenye hamu ya kumwaga damu. Hatakubali cho chote kiwe mbele yake. Ni mwingi wa hasira na tamaa ya uongozi. Hawajali watu. Hana huruma. Anaishi tu ile aweze kutawala na kutamalaki ulimwenguni kote.
Atafanya uharibifu ili awape nguvu watu wake. Hakuna kitakacho mzuia hadi nirudi kumsimamisha. Hakuna mwanadamu yeyote awezaye kumsimamisha ila mimi.
2 Wathesolonike 2:8. Hapo ndipo atakapofurushwa Yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake.
Nyakati za uovu zaja. Mipango ya mfumo huu kuanza inafanywa kisirisiri.
Watakao baki baada ya kanisa kunyakuliwa watatambua kuwa wanatawaliwa na mfumo wa mpinga Kristo ambao ni wa kuangamiza.
Wakristo walio vuguvugu ambao wataachwa watatambua kile ambacho kitakuwa kimetukia. Majuto yatakuwa makuu. Wengi watamfuata mpinga Kristo kwa sababu njia ya kumfuata Mpinga Kristo itakuwa rahisi kuliko ya kutomfuata. Utakuwa wakati wa uchaguzi mgumu. Wengi watajua mioyoni mwao kile ambacho wanahitaji kufanya na kwa ajili ya ujasiri wao na tama ya kuona ufalme wangu, watafanya uchaguzi huo mgumu. Imani yao itawasaidia. Imani ya kumkataa mpinga Kristo na kunichagua mimi. Wengi hawatakuwa na imani hii pamoja na ujasiri huo.
Ufunuo 19:20. Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hali katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti.
Kweli wanangu, jitayarisheni ili muweze kuokolewa. Wakati umefika. Jitayarisheni. Mkingoja na kunitazamia. Macho yenu yanitazame mimi. Mimi ndio mlango….mlango wa kutoka…. Mlango wa kuepukia. Hivi karibuni nitaufunga mlango huu. Huu tu ndio utakaokuwa mlango wa kuepukia. Wakati umewadia.
Kanisa langu lafaa kujitayarisha.
Mathayo 25:10. Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
Mpinga Kristo yu pembeni. Anafanya matayarisho ya kushika usukani. Anatafuta kutawala duniani. Hakuna litakalomzuia. Ukatili ndio alama yake. Atatawala kwa hofu na ukatili. Hakuna anayeweza kumzuia duniani. Nguvu zake zinakuja kupitia kwa adui yangu. Yeye ndiye mwenye ukatili huo.
Msiyapuuze mambo haya. Muonayo ni udanganyifu. Mnadanganywa kuwa kila kitu ki shwari. Adui wangu ndiye anayewadanganya. Anataka kuwapoteza. Hawataki mtembee kwenye njia nyembamba ili mnijie na kuokoka.
Wanangu wamedanganyika kuwa kila kitu ki sawa. Yote si sawa wanangu! Yote si sawa! Dunia inatawanyika. Yafungueni macho yenu. Myakubali yanakuja kutukia. Amkeni! Tazameni! Someni neno langu na kulinganisha na yale yatendekayo kwa sasa.
Dunia inamkataa Mungu katika pande zote nne. Siwezi kuvumilia tena. Nauondoa mkono wangu wa ulinzi juu ya dunia, na kuiacha ifanye itakalo, bila mimi Mungu, Muumba wake.
Mimi ni Mungu anayeelewa bali dunia ikinitaka niondoke na kusimama kando, hivyo ndivyo nitakavyofanya. Ndipo mtakapogundua kuwa bila mkono wangu wa ulinzi, mambo ni tofauti. Ni mvumilivu, lakini sasa uvumilivu wangu umefika kikomo. Wanangu, nawasihi… tafadhali njooni kwangu. Jitoleeni kwangu kikamilifu.
Nipeni maisha yenu. Nitayakubali. Nitawafunika na damu yangu. Nitawaosha kwa neno langu. Wakati umefika. Mnahitaji kusafishwa ili muweze kuja nami nitakapokuja kumchukua bi arusi. Mngali mna nafasi. Jitayarisheni. Muda umekwisha. Hakuna kitakachonizuia.
NI mimi YAHUSHUA….. MFALME MKUU… MUNGU MNYENYEKEVU.
Yohana Mtakatifu 15:3. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.
SURA YA 18: MUDA WA KUSHUKA KWANGU UMEFIKA
Natuanze tena. Sasa ni wakati wangu kuzungumzia juu ya mada mpya: Wana, muda wangu wakushuka chini umefika.Wengi hwajajitayarisha na wengi wana anguka. Wengi
Comments (0)