bookssland.com » Religion » Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) - Susan Davis (free ebook reader for iphone .TXT) 📗

Book online «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) - Susan Davis (free ebook reader for iphone .TXT) 📗». Author Susan Davis



1 ... 4 5 6 7 8 9 10 11 12 ... 17
Go to page:
Bado kuna matumaini. Wanangu, njooni kwa mikono ya kuaminika. Nawajali. Nawapenda. Ni tayari kuwafunza bila kujali yale ambayo mumetenda au bila kujali mtokako. Njooni! Njooni! Huu ndio wakati wa wokovu. Msifuate dunia ambayo inaangamia kwa sababu ya kumkataa Mungu mmoja mwenye ukweli na njia zangu nyoofu.

Wengi watakawia sana na baadaye watajuta kuhusu uamuzi wao. Msiache haya yawatendekee. Ni tayari kuwapa moyo wangu. Kuwa wazi nanyi. Kuwaleta kwangu na kushiriki nanyi kwa undani. Hili ndilo tamanio langu: Kuwainua na kuwakinga kwa wakati mgumu. Nawaomba mniache nishiriki nanyi nyakati zenu ngumu. Nataka mniruhusu niwafariji. Natamani kuwa na uhusiano wa namna hii nanyi. O! Nitamanivyo! Msinisukume mbali, mimi muumba wenu. Yakubali niwaambiayo. Nataka niwe karibu nanyi; karibu sana kuliko vile mtu mwingine ye yote yule awezavyo. Nawapa wanangu uhusiano ambao ulimwengu hauwezi kuwapa. Hakuna binadamu awezaye kuwa na uhusiano kama huu na nanyi. Nataka muwe na uhusiano wa ndani nami muumba wenu awajuaye kuliko ye yote yule. Nawapa uhusiano huu wa karibu. Nawapa moyo wangu. Ni wangu kuwapa na ninawapa. Ni wenu ikiwa mtauliza. Ni wachache sana wanaoniuliza, bali upo. Wanangu, nafungua moyo wangu na kuwaalika mje ndani, mnifurahie. Njooni mnijue sana kwa undani, kiliko kuniona kama Mungu aliye mbali nanyi. Mnaweza kunijia. Naweza kuwaambia mawazo yangu niliyonayo juu yenu. Naweza kuwafariji, niwaongoze katika nyakati za matatizo na kuwahimiza wakati munapitia mashaka. Mimi ni Mungu wa upendo. Ni tayari kuwa karibu nanyi. Tutembee pamoja katika maisha haya. Hamtawahi kutembea pekee yenu tena. Ni kando yenu. Kuwaliwaza, kuwashikilia na kuwahimiza. Njooni mnijue katika uhusiano huu ambao nimetamani kushiriki nanyi siku zote.

Niliuumba kwa ajili hii, muwe na uhusiano wa ndani nami. Ndio azma yako maishani. Hata msiponiamini, mimi ndiye muumba wako na hivyo ndivyo ilivyo. Natamani kuwa nanyi wakati mu chini na wakati mu juu. Wakati wa huzuni na wakati wa furaha. Tushiriki maisha pamoja, tutembee katika njia nyoofu pamoja. Haya ndiyo maisha niliyowapangia. Mpango wangu kmamilifu, na mapenzi yangu kwa maisha yenu.

Zaburi 139:3. Umepepeta kwenda kwanguna kulala kwangu. Umeelewa na njia zangu zote.

Kwa hivyo, njooni kwangu. Nitoleeni maisha yenu. Niacheni kwa unyenyekevu, nami nitayachukua, niyasafishena kuyatayarisha kwa ufalme wangu ili mshiriki kwa karamu ya ndoa yangu kama bi arusi wangu. Mkiniuliza nitawapa haya yote. Natamani kuwaweka duniani mwangu. Mimi Mungu ni tayari na ninawasubiri. Acheni kuishi maisha yenu mbali na muumba wenu.

 

 

SURA YA 13: WANANGU, MUDA UNAYOYOMA

 Sasa, hebu tuanze. Wanangu. Nazungumza na wanangu: Muda unayoyoma. Naja kwa kasi kwa mabawa ya njiwa weupe, kwa farasi wa kifahari, nikiwa nimezungukwa na mamilioni ya malaika. Siku hii inakaribia. Mnahitaji kuwa tayari, mkingoja na kukesha, mkinitazamia.

2 Wathesalonike 3:5. Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.

Huwa sichelewi. Mimi huja kwa wakati. Neno langu ni njema. Natenda ninavyosema na kwa wakati. Wakati wa kufunga umewadia. Kwa hivyo wale ambao mnanisubiri, msife moyo. Mimi ni Mungu anayetimiza neno lake. Neno langu ni njema na thabiti. Mimi ni Mwamba! Hakuna awekaye imani yake kwangu atakosa kuridhika. Hakuna! Sibadiliki. Mimi ni yule yule jana, leo na hata milele. Mimi ni Alfa na Omega! Wanangu, jitayarisheni! Wekeni kando mambo yote ya kidunia na mjitayarishe. Mtajitayarishaje?

Nataka mnyenyekee kwa utiivu.

Nataka toba ya kweli mkinyenyekea na kukiri dhambi zenu mbele ya Mungu Mtakatifu, mnayewajibika kwake.

Nataka mjitolee kikamilifu bila kusita.

Nataka muiweke imani yenu yote kwangu.

Nataka mjazwe na Roho wangu Mtakatifu. Njooni mpokee taa iliyojaa mafuta.

Nataka mjioshe kwenye neno langu na mjisafishe na damu yangu— damu niliyotoa kama fidia.

Nataka mnitafute kwa njia zenu zote na mnijue katika mahali pa siri.

Nataka mtembee nami kila siku na kunitegemea kila wakati.

Nataka muombe kwangu na kuzungumza nami siku yote.

Huyu ni Bwana wenu anayenena nanyi. Wanangu, nawataka muwe macho, mkinitazamia. Nataka mzione dalili, mzitambue siku na kukisoma kitabu changu. Msikose kuujua ukweli. Huu ni wakati mbaya na hautakuwa mwema. Hakuna wema unaokuja duniani, ni mambo ya kutisha tu. Nisikizeni vyema: Ukweli wangu kila wakati ni wa kuaminika. Mnaweza kuutegemea. Nilinena hapo awali kuhusu matukio yajayo na sasa yamewadia. Wana, huu si wakati wakuwa walegevu na kupenda kulala. Amkeni! Njooni kwa ukweli wangu. Jirekebisheni! Nawasubiri. Achilieni dunia! Hii dunia ambayo mnaiamini kwa moyo wote. Msikwamilie dunia ambayo inasambaratika. Haitawapa majibu. Acheni kubwata kati yangu na dunia. Siwezi kukubali kujitolea nusu nusu. Sitakubali kamwe. Ni lazima mje kwangu kikamilifu. Bila hivyo haiwezekani. Wanangu, niliwafia kifo kikamilifu na cha aibu. Nilijitolea kufa bila kuzuia chochote kutendeka kwangu. Sikukimbia ili nizuie kifo changu kwa ajili ya dhambi zenu. Nilipata wakati mgumu. Kila dakika ilikuwa ya mateso. Nilikuwa kama mwana kondoo kwa mbwa. Nililipa deni lote.

Zaburi 22:16. Kwa maana mbwa wamenizunguka; kusanyiko la waovu wamenisonga; wamenizua mikono na miguu.

Msikane deni hili kubwa nililolipa kwa ajili ya adhabu zenu. Mkikataa niwapayo, hamtapata tena msamaha mwingine wa dhambi zenu. Hakuna msamaha mwingine tena wa dhambi. Ingawa watu wanautafuta, haupo. Mimi ndiye malipo ya hilo deni: Damu yangu iliyomwagika. Mateso yangu msalabani. Mwili wangu uliovunjika. Moyo wangu uliovunjika. Nililipa deni lenu. Nanilifanya hivyo kwa hiari yangu ili mpate kuwa na uhusiano bora nami, Baba yangu, na Roho Mtakatifu. Haya ndiyo niliyoyapitia na hiyo ndiyo sababu ya kuyapitia.

Waebrania 13:12. Kwa ajili hii, Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe aliteswa nje ya lango.

Hii ni zawadi yenye tunu. Wanangu, thamana haiwezi kuwekwa kwenye zawadi hii. Hakuna thamana inayotosha. Msiifanyie mzaha na kuiona bila maana. Ipeni heshima zawadi hii. Hakuna zawadi nyingine kutoka kwaMungu zaidi ya hii.

Sasa wana, sitaki malipo ya zawadi hii. Hakuna malipo yanayoweza kutosheleza kulipia zawadi hii. Nawapa bure. Muichukue bila malipo. Msikatae zawadi kuu kama hii kutoka kwa Mungu aliye mnyenyekevu na mkarimu. Kuikataa zawadi kuu kama hii kutasababisha adhabu ya milele. Kukataa zawadi kuu kama hii kutafanya uende jehanamu. Je wanangu, hamunielewi? Msiifanyie zawadi hii mzaha. Muilinde vyema kwa maana ni tunu kubwa kutoka kwa Mungu kwa ajili ya wokovu wenu na uhuru wa milele kuwatoa jehanamu.

Waebrania 10:29. Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyokubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema.

Hii ni zawadi isiyo na kifani. Ni wachache sana hapa duniani wanaoithamini. Ni wachache sana watakaotembea kwenye barabara za dhahabu, kwa ajili ya dharau walionayo juu ya zawadi yangu kubwa kwa wanadamu. Msidanganywe. Kuikejeli zawadi kubwa kama hii ni balaa. Ishikilieni, ithaminini, na kuiheshimu zawadi yangu na kuifurahia kwa maana ni kupitia kwa zawadi hii ndio mtapokea wokovu wa milele, tumaini, na uzima wa milele katika ufalme mkuu wa Mungu. Zawadi yangu kwa wanadamu ambayo ni mimi tu ningeweza kuilipia na mimi tu ningeweza kutimiza yale ambayo mwingine hangeweza. Nawapa pendo langu bure. Pendo langu lililo kuu kuliko pendo lingine lolote lile. Njooni mle nami kwenye meza ya upendo na mpate upendo usiolinganishwa na mwingine. Nawapa bure. Hakutakuwa na wakati mwingine. Utwaeni --- twaeni bure bila malipo. Ni upendo ulioko kila wakati. Huu ni upendo wangu ninaotoa kama dhabihu kwa wote.Ye yote yule awezaye na aje ...

BWANA YAHUSHUA, MFALME MKUU,

MWANA-KONDOO MNYENYEKEVU, DHABIHU ILIYOMWAGIKA

 

SURA YA 14: DUNIA IMENIGEUKA

Natuanze, mwanangu. Wanangu ninataka kuizungumzia dunia ambayo imenigeuka. Dunia hii imenigeuka mimi pamoja na yote yale ninasimamia. Imekua mbovu na isiyokalika.

Yakobo 4:4. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adhi mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

Wanangu, dunia imejawa na dhambi. Hakuna unapoweza kupata ukweli na utakatifu. Hata makanisa yangu ya mbali nami. Hata wale wanaodai kunijua wa mbali nami. Wananiweka mbali. Hata viongozi wangu hawapati ushauri kutoka kwangu. Hawanitafuti. Hawanijui. Makanisa yamekuwa maficho ya uasi kwa maana wanahubiri maubiri ya uongo. Hawanijui wala kutaka kunijua. Mimi ni Mungu asiyefahamika kwao.

Dunia haina wakati na Mungu wao. Inamtafuta tu kwa maneno wala sio kwa ukweli. Dunia imejaa waongo na wezi, watu wenye majivuno na waabudu sanamu wanaofuata dunia na mambo ya kidunia, wala sio mimi Mungu wake.

Ni huzuni ulioje kwa wale wasionifahamu bali wanasema na kudhani wananifahamu. Mimi ni Mungu anayeweza kufahamika. Sijajificha kwa wale wanaonifuata. Mimi siye Mungu asiyefahamika kwa wale wanaonikaribia kwa unyenyekevu. Nafahamika. Nikaribie nami nitakukaribia.

Zaburi 73:28. Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; nimefanya kimbilio kwa Bwana Mungu, niyahubiri matendo yako yote.

Wanangu kila uendako, uovu upo. Hakuna cho chote duniani ambacho adui hajatengeneza kwa minajili ya kuwafanya mkose kuwa karibu nami MUNGU. Mfumo wote wa dunia niwakuhakikisha kuwa wanangu wa mbali nami. Ikiwa adui yangu atawafanya mfuate miungu mingine basi hamtaweza kunitafuta na kuipata njia ya ukweli ili mpokee wokovu wangu, utakatifu wangu, na uhuru wangu.

Huu ni mpango wa adui wakuwafanya mkose kufahamu na mpoteze mahali penu katika ufalme wangu. Mfumo huu wa dunia umewekwa pamoja na mipango ya adui wangu. Kila kitu ni cha ubinafsi wala sio kwa mpango au mapenzi ya Mungu, wala kutafuta Mungu. Adui hataki mje kunitafuta. Anataka mfungwe kwenye mfumo wa ubinafsi unaowafunza kujifikiria tu wenyewe bila kuwajali wenzenu. Anataka ujifikirie tu, ujitegemee, na kujipangia siku zako za usoni mwenyewe bila kumtegemea Mungu.

Hii siyo njia yangu wanangu. Mapenzi yangu yanasema unitafute na kunifuata mimi, unitegemee, ufuate njia zangu. Unapojitafutia mapenzi yako na hiari yako u nje ya mapenzi yangu na hiyo ni dhambi. Unaishi dhambini ikiwa u nje ya mapenzi yangu. Utajuaje mapenzi yangu juu ya maisha yako ikiwa hunitafuti wala kujitolea kwangu kikamilifu? Ni sharti uiweke kando mipango yako, njia zako na uniruhusu kukuelekeza maishani mwako. Ni katika tu kutembea ndani ya mapenzi yangu maishani mwako ndipo utapata uhuru na amani, amani nikupayo. Kufuata njia zako mbali nami itakuangamiza. Hautaweza kushinda dhambi. Mapenzi yangu ni wingi wa Roho Mtakatifu na kuwa na taa iliyojaa mafuta. Hivi ndivyo utakavyo kuwa tayari kwa kurudi kwangu, uokolewe na kupelekwa mahali salama.

Wanangu, amkeni! Huu ndio ukweli! Hakuna ukweli mwingine!

Mathayo Mtakatifu 25:4. Bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao na taa zao.

 

 

SURA YA 15: VIONGOZI HAWANIFUATI

Natuanze tena. Wanangu, ninasononeka juu ya dunia hii ambayo hainijali. Siheshimiwi hata kidogo. Watu wangu hawanitafuti -- wale ambao nimewaita ili kuwaongoza kondoo wangu. Wana mipango yao wenyewe na hawatafuti ushauri kutoka kwangu. Siwezi kuwategemea. Hawawambii watu ukweli, ila tu yale wanayoamini kuwa watu wanataka kusikia.

Watu wangu hawana

1 ... 4 5 6 7 8 9 10 11 12 ... 17
Go to page:

Free e-book «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) - Susan Davis (free ebook reader for iphone .TXT) 📗» - read online now

Comments (0)

There are no comments yet. You can be the first!
Add a comment