Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) - Susan Davis (free ebook reader for iphone .TXT) 📗
- Author: Susan Davis
Book online «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) - Susan Davis (free ebook reader for iphone .TXT) 📗». Author Susan Davis
Huyu ni BWANA wenu YAHUSHUA. Ni mvumilivu nikiwasubiri muamue. Nichagueni ili mwokolewe!
SURA YA 38: WAFUASI WANGU KAMILI WANANITAZAMIA — WAMEJIHADHARI.
Binti, natuanze. Binti yangu, ni tayari kukupa maneno mapya: Wana, huyu ni BWANA anayezungumza nanyi. Saa imewadia ya kurudi kwangu na wanangu wamelala fofofo. Hawajijui wala hawajui yanayoendelea kando yao. Hata hawanitazamii. Ni wazi kuwa ni vipofu na macho yao hayako kwangu. Nitakuja kama mwizi usiku. Wengi watapatwa bila kujihadhari. Je, neno langu halisemi hivi? Ikiwa ni hivyo, mbona wengi wenu mnalipuuza? Mbona mnakataa kukesha na kuomba? Nawapa yaliyo mema nanyi mnanifanya wa mwisho maishani mwenu. Kama wanangu wangalikuwa wananifuata kwa karibu, wangalijua kuwa huu ni wakati wa kunitazamia, kunitafuta na kunisubiria. Wangeutambua ulimwengu ambao umewazunguka, na jinsi dunia inavyoendelea kunikataa katika pembe zote nne. Wafuasi wangu kamili wananitazamia. Wamejihadhari. Wametega masikio wanasikiza sauti ya hatua zangu. Wanatazama mienendo yangu yote na kusikia sauti yangu. Naja na hili sio jambo geni kwa wale wanaonitazamia. Hawa wana ni wavumilivu na wananingojea kwa hamu. Hili ndilo kanisa langu, bi arusi wangu. Yuapendeza na shauku yake juu ya kurudi kwangu inanipendeza. Napenda jinsi alivyo na hamu akiningojea. Huyu ndiye niliyemfia. Wafuasi wangu waminifu wanaoua ubinafsi wao na tamaa zao ili kuniishia mimi.
Luka Mtakatifu 12:37. Heri watumwa wale ambao Bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amini nawambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
Wanayaweka maisha yao miguuni pangu na kuyaacha mambo ya dunia na kufuata Mungu wao. Nawashukuru sana kwa haya yote na zawadi zao hazitakwisha. Hili ndilo kanisa langu. Mwaweza kuwa mmoja wa kanisa hili, bi arusi wangu. Mwaweza kujitayarisha ili nikija niwachukue niwapeleke kwenye makao yenu huko mbinguni ambayo nimewaandalia. Wakati ulioko ni mfupi sana kwa hivyo muweke bidii ya kunifuata. Nataka mjitolee kote kote. Nataka mnipe maisha yenu na kila kitu chenu. Msiache chochote. Nayataka maisha yenu yote. Nitawabadilisha na kuwapa maisha mapya ndani yangu. Nitawaosha na damu yangu muwe wasafi na niwajenge katika ufalme wangu; niwape nafasi kati ya wanangu ambao watanitumikia milele; wataishi na kutawala nami milele, kando yangu. Huyu ndiye bi arusi wangu. Ni mrembo. Watu waliojiandaa na kujitayarisha, wakikesha na kungojea MFALME wao. Naja kuwaokoa hawa wana, niwapeleke katika uhuru na usalama mbali na uovu ambao utaikumba dunia. Hawa ndio washindi wangu. Mwaweza kuwa miongoni mwao. Nawasubiri wanangu ili mje mshiriki katika karamu ya harusi yangu, muwe kati ya wale walio kwa ufalme Mungu. Nimewawekea nafasi katika meza yangu ya karamu ya ndoa yangu. Ni mahali ambapo nimewawekea ila ni lazima ninyi wenyewe kupadai. Sitaufungua mlango milele. Hivi karibuni, wanangu watapita kwenye mlango huu kisha nitaunfunga na kuwaacha wale waliokataa mwaliko wangu nje, wakabiliane na maovu yajayo. Itakuwa siku ya huzuni ilioje kwa wale wanaokataa kukubali maneno yangu! Watakapogundua kuwa wameachwa watakuwa na mahangaiko makubwa. Ndipo watakapojua kile ambacho wamekosa na yale ambayo wanaenda kukumbana nayo. Kutakuwa na majuto. Kutakuwa na kilio wakati kanisa langu vuguvugu litatambua makosa yake ya kukataa kuyasikiza maonyo yangu. Ndiyo, kutakuwa na simanzi kuu, watakapogundua kuwa wamepoteza nafasi yao katika ufalme wangu. Msiachwe ili mshuhudie giza litakalokuja duniani. Njooni kwangu. Jitoleeni kwangu, tubuni dhambi zenu zote mkijuta dhambi zenu na kuwa na tamaa ya kunifuata kwa mioyo yenu yote. Nitaibadilisha mioyo yenu na kuziosha dhambi zenu muwe wasafi kwa damu yangu. Hivyo mtasimama mbele yangu mkiwa mumejiandaa na kuwa tayari kushiriki kwenye karamu ya ndoa yangu kuu. Hii ndiyo hamu kuu niliyo nayo moyoni mwangu. Mnirudie. Mimi ni BABA yenu, MUUMBA wenu. Natamani mnijie ili niwafanye muwe wanangu wa kiume na kike. Mna nafasi sasa hivi ya kujirekebisha mbele zangu. Njooni ili tuishi wote milele. Naungojea uamuzi wenu.
Ni mimi BWANA wenu, MFALME wenu, MUNGU wenu, JEHOVA.
SURA YA 39: USHUHUDA WANGU KUHUSU KITABU HIKI NA KUFUNGA KWANGU
Bwana aliniita na kuniambia niende mahali pa faragha ili niombe na kufunga bila kula bali ninywe maji pekee. Baada ya wiki mbili, nilishiriki katika meza ya Bwana kila siku, kisha baadaye nikunywa maji ya machungwa glasi nne kila siku. Kufunga huku hakukuwa rahisi kwangu. Ni jambo ngumu sana ambalo nilitenda maishani mwangu. BWANA alinileta mahali hapa ili nijikane mwenyewe na tamaa zangu. Pia alinipa maneno ambayo nimeyaandika ili wengine wapate nafasi ya kuyasoma. Maneno niliyoyaandika hapa, Mungu aliyasema kwa sauti huku nikiyaandika. Ilikuwa mnamo mwaka wa 2012 kuanzia Januari 27, 2012 hadi Machi 6, 2012. Kuna barua zingine ambazo sikuweka tarehe kwa maana kwangu maneno haya yalikuwa muhimu kuliko tarehe. Wakati wa kufunga, Mungu aliniambia kuwa nikihisi njaa nimuulize anipe “Mkate wa Mbinguni.” Kwa hivyo kila wakati nilipohisi njaa, niliomba na kumuuliza anipe “Mkate wa Mbinguni” na mara tu maumivu ya njaa yalikwisha. Kweli MUNGU ni mkate utokao mbinguni.
Wakati mmoja nilikuwa nikisoma kitabu ambacho kilinifanya niamke. Kiliandikwa na mwanamke mmoja ambaye Mungu alikuwa amemuonyesha mbinguni na jehanamu. Na alisema kuwa katika jehanamu, watu daima wanahisi njaa na kiu. Nikajiuliza, “Ikiwa watu hawa watakuwa na kiu na njaa milele, mbona naona ugumu wa kufunga siku arobaini tu na angalau ninakunywa maji?” Tangu siku hiyo, niliweka bidii maana sikutaka kwenda jehanamu na kuishi huko milele nikihisi njaa na kiu. Nawataka ninyi pia mfikirie sana juu ya maisha yenu ya milele. Myatilie maanani maneno haya. Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kumaliza mfungo huu wa siku arobaini.
Kuhusu maneno haya, MUNGU alitumia maneno mengi ambayo hata mimi mwenyewe sikujua maana yake lakini wakati nilipoyatizama kwenye kamusi, nikayapata na yalikuwa sawa kabisa na vile alivyotaka niandike. Hakuna hata mabadiliko yo yote niliyofanya katika kitabu hiki. Yote yale MUNGU aliniambia niliyaandika vivyo hivyo.
UTUKUFU KWA NUNGU! ASANTE BWANA kwa uvumilivu wako juu ya chombo hiki kisicho na maana, Susan Davis.
YESU NDIYE MKATE KUTOKA MBINGUNI
Yohana Mtakatifu 6:29-58. 29 Yesu akawajibu, “Kazi anayotaka Mungu muifanye ni hii: mumwamini yeye aliyenituma.” 30 Wakamwambia, “Utafanya ishara gani ya muujiza, tuone ili tukuamini? Utafanya jambo gani? 31 Baba zetu walikula mana jangwani. Kama Maandiko yanavyosema, ‘Aliwapa mikate kutoka mbinguni wakala.”’
32 Yesu akawajibu, “Nawaambia kweli sio Musa aliyewapa mkate kutoka mbinguni. Baba yangu ndiye anayewapa mkate wa kweli kutoka mbinguni. 33 Kwa maana mkate wa Mungu ni yule aliyeshuka kutoka mbinguni na ambaye anatoa uzima kwa ulimwengu.”
34 Wakamwambia, “Bwana, tupatie mkate huo sasa na siku zote.
35 Yesu akawaambia, “Mimi ndiye mkate wa uzima. Ye yote ajaye kwangu hataona njaa kamwe, na ye yote aniaminiye, hataona kiu kamwe. 36 Lakini kama nilivyokwisha waambia, mnaniona lakini bado hamtaki kuamini. 37 Wale wote ambao Baba amenipa watakuja kwangu na ye yote ajaye kwangu, sitamtupa nje kamwe. 38 Kwa maana sikushuka kutoka mbinguni nije kutimiza mapenzi yangu, bali nitimize mapenzi yake yeye aliyenituma. 39 Na mapenzi yake yeye aliyenituma ni haya: kwamba nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa bali niwafufue wote siku ya mwisho. 40 Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni haya: wote wamwonao Mwana na kumwamini wawe na uzima wa milele. Nami nitawafufua siku ya mwisho.”
41 Wayahudi wakaanza kunung’unika kwa kuwa alisema: “Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni.” 42 Wakasema, “Huyu si Yesu mwana wa Yusufu? Na baba yake na mama yake si tunawajua? Anawezaje basi kutuambia kwamba ameshuka kutoka mbinguni?”
43 Lakini Yesu akawaambia, “Acheni kunung’unika. 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama Baba aliyenituma hakumvuta kwangu; nami nitamfufua siku ya mwisho. 45 Kama manabii walivyoandika, ‘Wote watafundishwa na Mungu.’ Ye yote amsikilizaye Baba na kuji funza kutoka kwake, huja kwangu. 46 Hii haina maana kwamba kuna mtu aliyekwisha kumwona Baba. Ni yule aliyetoka kwa Mungu peke yake, ndiye aliyekwisha kumwona Baba. 47 Nawaambieni kweli: anayeamini anao uzima wa milele. 48 Mimi ni mkate wa uzima. 49 Baba zenu walikula mana jangwani, wakafa. 50 Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni ambao mtu ye yote akiula, hatakufa. 51 Mimi ni mkate wa uzima uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu ataishi milele. Na mkate wenyewe ni mwili wangu ambao nitautoa ili watu wote ulimwenguni wapate kuishi milele.”
52 Hapo Wayahudi wakaanza kubishana kwa hasira wakiulizana, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?”
53 Kwa hiyo Yesu akasema, “Ninawaambieni hakika, msipoula mwili wangu mimi Mwana wa Adamu na kuinywa damu yangu, hamtakuwa na uzima ndani yenu. 54 Mtu ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 55 Kwa maana mwili wangu ni chakula halisi na damu yangu ni kinywaji halisi. 56 Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu anaishi ndani yangu na mimi ninaishi ndani yake. 57 Kama vile Baba wa uzima alivyonituma, na kama nipatavyo uzima kutoka kwake, kadhalika, ye yote anilaye ataishi kwa sababu yangu. 58 Huu ndio mkate uliotoka mbinguni, si kama ule mkate walio kula baba zenu hatimaye wakafa. Alaye mkate huu ataishi milele.” 59 Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sinagogi huko Kapernaumu.
Imprint
Publication Date: 03-02-2016
All Rights Reserved
Comments (0)