Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) - Susan Davis (free ebook reader for iphone .TXT) 📗
- Author: Susan Davis
Book online «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) - Susan Davis (free ebook reader for iphone .TXT) 📗». Author Susan Davis
1 Yohana 1:7. Bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisisha dhambi yote.
Natuanze, binti. Leo nataka kuzungumzia juu ya wale watakaoachua wakati wa unyakuo.
Baada ya unyakuo, dunia haitakuwa sawa tena. Kutakuwa na mageuzi makubwa mahali pote. Dunia haitakuwa sawa tena. Hofu kuu itakuwa duniani. Wanangu walio vuguvugu wataelewa kile ambacho kimetendeka na hofu, hofu kuu, itawaingia moyoni.
Dunia haitatenda mambo kama kawaida. Hata ya nchi itageuka. Kutakuwa na mioto na majanga makuu mahali pote. Watu watakuwa bila ulinzi kwa sababu vikundi vya watu wenye ghasia watakuwa wakitembea pote wakitafuta watu wakuvamia na kuwanyang’anya walivyo navyo. Hakutakuwa na askari au polisi wa kuwasaidia kwa maana kutakuwa na vurugu.
Wengi watayapoteza maisha yao kwa sababu uharibifu wa ghafula utaikumba dunia. Mahali pote duniani hapatakuwa sawa tena kwa maana watu wengi wataangamia mara moja.
1 Wathesalonike 5:3. Wakati wasemapo, kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
Hofu kubwa itawangia watu kote duniani. Hakutakuwa na pahali pa usalama pakwenda. Hakutakuwa na chakula. Watu watakata tamaa. Haya yataendelea kwa muda fulani ndipo mpinga Kristo ataingia na kuiweka dunia nzima chini ya mamlaka yake.
Mwanzoni, watu wataona kama ni jambo njema kwa sababu dunia itatulia, ila utulivu anaouleta utakuwa ni kifo kwa wengi. Watakaokataa mfumo wake wata uawa, na wengi watateswa na kusumbuliwa. Kuukata mfumo huu hakutakuwa kwema kwa maana hatamvumilia yeyote. Yeye ni muovu kabisa. Atauweka ulimwengu wote chini ya utawala wake wa udhalimu. Nchi zote zitamfuata kwa kutaka kuweko kwa mpangilio baada ya machafuko yaliyoachwa na unyakuo.
Huu utakuwa wakati wa huzuni kwa ulimwengu wote. Wengi watajiua wakitafuta kuepuka. Huu hautakuwa utatuzi kwa hivyo mtu ye yote asifikirie hata kuyachukua maisha yake.
Mpinga Kristo ataweka chapa ya mnyama kama njia ya kuwatawala -- kuikataa chapa au alama kutakuhukumia kifo. Hakuna atakayeachwa.
Ufunuo wa Yohana 13:16-17. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kiume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
Ufunuo wa Yohana 14:11. Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.
Wafuasi wangu wengi walio vugurugu sasa wataelewa gharama ambayo ni sharti walipe ili waingie kwenye ufalme wangu. Wengi hawatamtii mpinga Kristo na kwa hivyo wengi watakufa kwa ajili ya imani yao. Watakuwa wengi.
Haijalishi ni wangapi watakaokufa kwa Mpinga Kristo. Tamaa yake ya kutaka kutawala itakuwa moyoni mwake. Hatajalii kuhusu wale watakaopoteza maisha yao. Utakuwa ni wakati mgumu kwa wale wanaolikiri jina langu. Ni wakati mgumu sana unaokaribia wanangu! Kumekuweko na nyakati ngumu ulimwenguni hapo nyuma bali huu wakati utakuwa mgumu zaidi. Hapa hapatakuwa pahali pema kwa aliye na watoto. Giza litatawala. Haya ndiyo yatakayolikumba kanisa langu vuguvugu.
Makanisa vuguvugu yatanirudia kwa wingi -- watu watanitafuta sana. Nitakuwepo bali lazima wapitie wakati mgumu. Familia zitatenganishwa na huzuni utatanda. Haya yote yatatokea kwa maana wanangu wamekuwa na mioyo migumu na kukataa kusikiliza maonyo ambayo nawapa kila siku. Haya yote yanaweza kuepukwa ikiwa wanangu watakuja kwangu, wanililie kwa mioyo minyenyekevu, watubu dhambi zao na kuutafuta uso wangu. Wajifunze kunijia kwa uhusiano wa karibu. Kimbieni mje kwa mikono yangu iliyo wazi kuwapokea. Nitawaonyesha ukweli kuhusu kurudi kwangu hivi karibuni na jinsi ya kujitayarisha kama bi arusi.
Njooni wanangu. Kimbieni. Nawasubiri ili niwaokoe kutoka kwa haya yote. Mimi ndiye muokoaji mkuu. Tamaa yangu ni kuwaokoa. Hakuna haja muachwe nyuma. Kuna nafasi kwa ye yote yule atakayekuja na kunitolea maisha yake. Nahitaji kujitolewa kwako kikamilifu na kutubu dhambi zako. Msidanganywe. Hakuna haja muachwe nyuma. Kuna nafasi kwa ye yote yule atakayekuja na kunitolea maisha yake. Nahitaji kujitolea kwenu kikamilifu na kutubu dhambi zenu. Msidanganywe. Hakuna njia nyingine. Niacheni niwaletee utulivu wakati wa unyakuo.
Natuanze tena. Wanangu wanadhani wana miaka mingi sana huko mbele. Hawaelewi kuwa nimechoshwa na huu ulimwengu.
Wanangu wameshikwa na dunia sana hata hawaoni jinsi dunia ilivyo mbali na ukweli ambao mimi Mungu nasimamia. Hata makanisa yao ya mbali na neno langu, ukweli wangu, kitabu changu. Viongozi wa makundi yangu wanajishughulisha na mambo ya dunia na wanaifanya kazi yangu kujifurahisha wenyewe. Hawana upendo kwangu. Wanafuata mali, umaarufu na kukubaliwa na walio wazunguka kisha wanaamini nita wabariki.
Wanaamini kuwa wingi wa watu makanisani mwao ndio kuonyesha kuwa wamefaulu na kwamba napendezwa na hayo. Ninapendezwa tu ikiwa viongozi wangu wanawaelekeza wafuasi wao kunitafuta mimi kwanza katika njia zao na kutembea nami katika uhusiano mtulivu. Ni wachache sana wanohuburi haya kwa sababu hawataki kuwaudhi wengi wanaowataka waje kwa makanisa yao. Wengi wanaleta pesa na pesa zinafanya kila mmoja afurahi bali ufalme wangu siowa utajiri katika maisha ya sasa.
Luka Mtakatifu 16:13. Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili, kwa maana ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
Viongozi wangu wa mbali nami. Na mbona wasiwe? Ikiwa wanataka kuwafurahisha, muda wao nami utatoka wapi? Wanaishi kwa sababu yangu! Mimi ndiye niletaye jua na mvua.
Huu ni wakati wa giza na giza linaendelea kuwa kubwa kila siku, ilhali viongozi wangu wanaendelea kuuficha ukweli huu kutoka kwa makundi yangu. Wanaficha ukweli nakuwaletea maneno ya furaha na raha. Makundi yangu yanadanganywa na hayatayarishwi. Wanadhani mambo yote ni sawa na wanaendelea kuishi maisha yao kama kawaida.
Ni maonyo yapi nitakayowapa ili niwaamshe? Ni lipi wanalotaka kusika ndipo wakiamini kitabu changu ambacho kimewapa ukweli? Hakuna asikiaye wala aminiye. Ni yapi yatakayosemwa kwa kanisa ili wayasikie maonyo na kuziweka kando tamaa zao za vitu vya dunia ili wakeshe na kujitayarisha?
Hosea 4:6. Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi, kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
Wamekuwa wapole na wanapotoshwa. Muda unayoyoma nalo kanisa linabaki limeridhika tu kana kwamba kila kitu ki sawasawa. Kanisa vuguvugu limedanganywa -- linanifuata bila uhai. Kanisa lingalinifuata na kuwa na uhusiano wa ndani nami, basi maonyo niwapayo hayangalikuwa mageni kwao na wangaliyafuata kwa moyo wote.
Huu ni wakati wa giza kuu kwa makanisa. Machache sana yanaelewa. Ni machache sana yanayotembea kwa njia zangu na maadili yangu. Neema haitapewa wale wanao asi kwa hiari, na wanao kataa kutubu. Mnamuhuzunisha Roho Mtakatifu wangu kisha mtafanya nini kanisa?
Waefeso 4:30. Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.
Mnapomfukuza Roho Mtakatifu wangu kutoka kwa hayo majumba yenu ya fahari eti kwa sababu amezidi kupita kiasi kumbukeni mimi na Roho wangu tu kitu kimoja. Mnamuabudu nani ikiwa mumemfukuza Roho Mtakatifu wangu kutoka mahali mlipo? Niambieni ni nani mnaye muabudu? Mnaabudu miungu wengine!
Matendo ya Mitume 7:51. Enyi wenye shingo ngumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; baba zenu walivyofanya, na nanyi ni vivyo hivyo.
Mumejiumbia Mungu wenu wenyewe. Mungu anayefaa tamaa zenu za kilimwengu, bali siyo Mungu mmoja aishiye milele. Ni kijimungu. Mwadhani kuwa wale watu wa zamani walioabudu sanamu za dhahabu walinikashifu sana. Nanyi vile vile hamna tofauti nao! Njooni kwangu mkinyenyekea kwa toba makanisa nami nitaziosha nafsi zenu. Nitawasamehe dhambi zenu za kuniacha na kukimbilia mali. Natamani kuwarudisheni, kwangu. Niacheni niwaamshe na kuwaletea amani na kuwaweka sawa na Mungu wenu.
Marko Mtakatifu 8:36. Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
Mambo yaliyo sasa, mu mbali nami na njia zangu. Siwezi kuwabariki. Naomba mnirudie O’ kanisa potevu! Ningali nasubiri muda kidogo. Kuchelewa sio chaguo. Simameni imara na kutii onyo hili. Tendeni! Maisha ya wengi yamo hatarini.
2 Timotheo 4:3-4. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watijipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti, nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
SURA YA 9: KUHUSU KANISA LILILOPOTEA
Natuanze. Katika neno hili, nataka kuzungumzia juu ya kanisa langu lilopotea; wale wanaoamini wa salama kwangu ilhali wa mbali nami. Nawazungumzia nyie sasa: wengi wamo katika makanisa wanayoamini yanawapa ukweli wote kunihusu na yale nisimamiayo -- lakini ukweli ni kwamba wamefanya neno langu kuwa hafifu. Hawawambii ukweli wote kikamilifu kwa sababu wengi hawataki ukweli. Hawawezi kustahamili ukweli. Hawataki kuijua injili yangu yote. Wanataka tu yale yanayopendeza masikio yao, ili waendelee kuishi kidunia na kuingilia anasa za dunia. Wakati wa kurudi kwangu umewadia na siwezi kuwachukua waumini wangu vuguvugu. Wataachwa nyuma. Ndipo watakapojuta kile imani yao hafifu imewatendea.
Ufunuo wa Yohana 3:15-16. Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una vuguvugu wala hu baridi wala moto, nitakutapika katika kinywa changu.
Sasa wanangu, hamwezi kutegemea viongozi wenu wa kanisa kuwapa ukweli. Ni lazima mnitafute ninyi wenyewe ndipo mpate ukweli wote. Lazima mkisome kitabu changu, mjitolee kwangu kwa moyo wote na mniulize niwajaze na roho wangu mkiwa na mioyo minyenyekevu na yenye kutubu. Hakuna njia nyingine. Nataka kujitolea kwote. Nitayabadilisha maisha yenu na maisha yaliyojaa wingi wangu na macho yenu yatafunguka kuona ukweli. Ukweli wangu. Ndipo mtaelewa ninachohitaji kutoka kwenu ili muweze kupokelewa ufalmeni mwangu.
Kanisa langu limepotea na wala halielewi maana ya kuwa mfuasi wangu. Hawafuati kanuni na njia zangu. Wanatafuta upenyo utakaowapa njia ya kutenda yale watakayo huku wakijisikia vema na kudhani kuwa wao ni wangu. Haya yamekuwa yakiendelea kwa muda mrefu sana na sasa yamezidi kiwango na ni wachache sana wanaotaka kuujua ukweli wote kikamilifu. Ni wachache sana wanaotamani kuelewa yale ambayo neno langu linasema.Wanataka hadithi ndogo ndogo zinazowafanya wajihisi vyema. Wanakuja na kwenda bila kunijali wala kutaka kujua mimi ni nani. Wanadhani wananijua. Wafuasi wangu wengi hawanijui. Wengi wanatapatapa kwa uhusiano wetu. Hawaelewi kikamilifu maana ya hao kunifanya Mungu wao. Mimi ni kama tu mtazamaji anayetazama maisha yao bila ya kushiriki kwa hayo maisha, bila kushiriki uhusiano wa ndani nao.
Mathayo Mtakatifu 7:21-23. Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Jambo hili linanihuzunisha sana kwa maana hii ndiyo sababu yangu mimi kuwaumba wanangu, wawe na uhusuani wa ndani nami, ili tutembee katika njia hii ya maisha pamoja. Ila dunia inawavutia hadi wanachagua njia iliyo duni badala ya kuja kwangu na kunijua mimi muumba wao. Huzuni kuu sana hii kukimbilia viumbe na kumkataa muumba; muumba wa vyote wanavyo kimbilia. Ni huzuni kuu kweli! Wanangu, hamuoni kuwa ninahitaji utakatifu na uaminifu? Nataka kuwa wazo lenu la kwanza, mpenzi wenu wa kwanza, nataka kuwa wa kwanza—kwa jumla. Hii ndio maana mliumbwa—muwe wenzi wangu milele. Ikiwa hamwezi kutembea nami kwenye njia hii sasa, mtawezaje kuwa wenzi wangu milele? Mtaunganishwa na nani milele? Mimi au adui wangu? Yafaa mjiulize swali hili wenyewe. Upendo wangu ni wa ndani sana kuliko upendo wo wote ambao mwanadamu anaujua. Msijiuze kwa kutafuta utoshelezaji duni. Hamtawahi kuujua upendo mkuu kuliko wangu. Wana, ipelelezeni mioyo yenu na kuzichunguza nafsi zenu. Tumesimamia wapi, Mimi nanyi? Tunapatana wapi maishani mwenu? Ni nje nikichungulia ndani au tu kwenye uhusiano? Ni mimi kiini cha maisha yenu? Mwanitaka niwe wapi? Jiulizeni. Nawasubiri. Mikono yangu i wazi kuwaleta kwenye uhusiano kamili na muumba wenu, Mungu wenu.
Muda unakaribia wa maamuzi muhimu. Je, ungependa kuwa kati ya bi arusi? Yeye ni wangu kwa jumla. Ananisubiri na kunitazamia. Mimi sio tu ndoto inayopita na ya muda mfupi
Comments (0)